• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wadau wa madini Dodoma watakiwa kukagua kumbukumbu

    (GMT+08:00) 2019-02-18 20:18:41

    Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula, ameagiza Ofisi ya Madini Dodoma kuitisha kikao cha wachimbaji wadogo wadogo kitakachokagua kumbukumbu za uzalishaji wao, ulipaji wa maduhuli na ushiriki wao katika huduma za kijamii.

    Prof. Kikula alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki alipofanya ziara katika kijiji cha Kwahemu wilayani Chamwino na kubaini kuwapo na idadi kubwa ya wachimbaji hao wa madini aina ya nikel milimani.

    Kwa upande wake, Ofisa Madini Dodoma Jonas Mwano, aliahidi kuitisha kikao haraka iwezekanavyo, huku akisema kuwa awali waliitisha kikao na wawekezaji wote waliulizwa wamefanya nini kwenye mrabaha wa serikali, huduma kwa jamii na tozo ya huduma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako