• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Mapato ya kahawa Kenya yapungua

    (GMT+08:00) 2019-02-19 18:51:47

    Mapato ya Kenya kutokana na kahawa yamepungua kwa asilimia 13 kwa kipindi cha miezi 4 iliopita ikilinganishwa na kipindi sawa na hicho mwaka jana.

    Hali hiyo imesababishwa na kushuka kwa bei ya kahawa aina ya Arabica kwenye soko la kimataifa.

    Taakwimu kutoka kwa mamlaka ya kahawa nchini humo zinaonyesha kuwa wakulima walipata dola milioni 41 kati ya Oktoba na Januari mwaka 2019 lakini kipindi sawa na hicho mwaka jana walipata dola milioni 47.

    Mkurugenzi mkuu wa soko la hisa la Nairobi Daniel Mbithi amesema kilo moja ya kahawa aina ya Arabica ilishuka bei kutoka shilingi 23 hadi 19 kwenye soko la kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako