• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Tanzania kukuza utalii kwa watu wa zaidi ya miaka 50

    (GMT+08:00) 2019-02-19 19:00:53

    Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, inatarajia kuanza mkakati maalumu wa kuongeza idadi ya watalii wenye umri mkubwa kuanzia miaka 50 na kuendelea.

    Mkakati huo pia utalenga kundi la watalii wenye bima za maisha zinazowaruhusu kusafiri na ndege kubwa zenye marubani wawili zitakazotua moja kwa moja kwenye hifadhi pamoja na wale wasioweza kusafiri kwa njia ya barabara kwa muda mrefu.

    Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu, amesema mambo yaliyomo katika mkakati huo ni pamoja na kuanzisha magari yatakayokuwa yakitembea kwenye nyaya (cable cars) kwa ajili ya kutumiwa na watalii wenye umri mkubwa kupanda Mlima Kilimanjaro ambao kutokana na umri wao hawawezi kupanda kwa njia ya kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako