• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi wa Tanzania wakamata muuaji wa mwanaharakati wa kupambana na ujangili

    (GMT+08:00) 2019-02-20 09:43:16

    Polisi wa Tanzania wamemkamata mtu aliyehusika na mauaji ya mwanaharakati wa kupambana na ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kwenye eneo la Manyara.

    Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Bw. Augustine Senga amesema polisi wamemkamata Bw. Limito Lebangu kutoka kijiji cha Limito Lebangu, kwa tuhuma za kuhusiana na mauaji ya kikatili ya mwenyekiti wa kijiji cha Gijedabung Bw. Faustine Sanka.

    Uchunguzi wa awali umeonesha kwamba, Bw. Sanka alikuwa akihimiza mapambano dhidi ya ujangili katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, na alifichua shughuli za ujangili za Bw. Lebangu na wenzake kwa walinzi wa Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, na hiyo ndio sababu ya kuuawa kwake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako