• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuwasaidia watu milioni 10 kuondokana na umaskini mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-02-20 18:05:44

    Mkutano wa baraza la serikali la China uliofanyika hivi karibuni umesema, mwaka huu China itawasaidia zaidi ya watu milioni 10, na wilaya 300 kuondokana na umaskini. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya uongozi wa kazi za kupunguza umaskini ya China Bw. Ou Qingping, amesema mwaka huu China itaendelea na juhudi za kupunguza umaskini, na kutatua matatizo ya kimsingi ya watu maskini, yakiwemo chakula, mavazi, elimu, matibabu na makazi.

    Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ufanyike, China imepata mafanikio makubwa katika juhudi za kupunguza umaskini. Mwaka jana China iliwasaidia watu milioni 13.86 kuondokana na umaskini, na kiwango cha watu maskini kilipungua kwa asilimia 1.43 ikilinganishwa na mwaka 2017. Kazi ya kupunguza umaskini haswa katika maeneo ya watu wa kabila la Watibet mikoani Tibet, Yunnan, Sichuan na Qinghai, na wilaya maskini zaidi mikoani Xinjiang, Sichuan, Yunnan na Gansu zimepiga hatua kubwa. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya uongozi wa kazi za kupunguza umaskini ya China Bw. Ou Qingping anasema,

    "Baada ya juhudi za mwaka mmoja, idadi ya watu maskini katika maeneo na wilaya hizo imepungua kwa watu milioni 1.34, na kiwango cha watu maskini kimepungua kwa asilimia 6.4, ambayo ni kubwa zaidi kuliko wastani wa sehemu zote za China."

    Bw. Ou amesema kuondoa umaskini katika sehemu maskini zaidi ni kazi muhimu na pia ni changamoto kubwa inayokabili China. Ingawa idadi ya watu maskini katika sehemu hizo si kubwa, lakini watu hao walioko katika mazingira magumu ya asili hawana uwezo wa kujiendeleza, hivyo ni vigumu kuwasaidia kuondokan na umaskini. Bw. Ou amesema serikali imetenga fedha zaidi kwa ajili ya sehemu hizo. Anasema,

    "Katika siku zijazo tutahimiza utekelezaji wa sera na hatua mbalimbali za kukabiliana na umaskini katika sehemu maskini zaidi, na kufuatilia, kuchunguza na kutathmini utekelezaji huo. Pia tutaendelea kusukuma mbele miradi ya kuboresha mazingira ya vijiji maskini, na kuwasaidia watu kutatua matatizo magumu."

    Bw. Ou amesema huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na pia ni mwaka muhimu wa ushindi katika vita ya kupunguza umaskini. Ameongeza kuwa lengo la mwaka huu ni kuwasaidia zaidi ya watu milioni 10 na wilaya 300 kuondokana na umaskini, na kutimia kwa lengo hilo ni msingi imara wa China kushinda vita ya kupunguza umaskini hadi mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako