• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa Umoja wa Mataifa asema majadiliano ndio njia pekee ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini Burundi

    (GMT+08:00) 2019-02-20 18:26:21

    Mjumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi Bw. Michael Kafando amesema majadiliano ndio njia pekee ya kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, na kufanya uchaguzi mkuu kwa amani mwaka ujao.

    Akizungumza jana kwenye kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya sasa ya Burundi, Bw. Kafalo amesema rais Pierre Nkurunziza wa Burundi ameeleza nia ya kugombea tena nafasi hiyo na serikali kukitambua chama cha upinzani cha National Congress for Freedom. Amesema hatua hizo ni mwelekeo mzuri na zinaweza kuchangia katika kufungua zaidi uwanja wa kisiasa.

    Wakati huohuo, Bw. Kafalo amesema vyama vya upinzani nchini Burundi vimeuomba Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kusimamia majadiliano ya amani ya nchi hiyo. Hivi sasa, majadiliano hayo yanaongozwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya rais Yoweri Museveni wa Uganda na na kusimamiwa na rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako