• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China haitavumilia uhalifu dhidi ya wanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka

    (GMT+08:00) 2019-02-20 18:32:05

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, serikali ya China haitavumilia uhalifu dhidi ya wanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka na biashara haramu, na kusema adhabu kali itatolewa kwa wahalifu husika kwa mujibu wa sheria.

    Bw. Geng Shuang amesema, kuanzia mwaka 2015, China imeweka vizuizi dhidi ya kuagiza bidhaa za pembe za Ndovu kutoka nchi za nje, na biashara na utengenezaji wa pembe hizo nchini. Amesema serikali ya China inawataka wananchi wake wanaoishi nchi za nje kufuata sheria za nchi husika, na haitasamehe uhalifu utakaofanywa na wananchi wake. Bw. Geng Shuang amesema China inaunga mkono idara husika za Tanzania kushughulikia kesi ya mfanyabiashara wa China Bibi Yang Fenglan, na kusema China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa ikiwemo Tanzania, kuendelea kutoa mchango kwa ajili ya kulinda wanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka na kuzuia biashara haramu.

    Mfanyabiashara wa China Bibi Yang Fenglan amehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela kutokana na kosa la kufanya biashara haramu ya pembe za Ndovu karibu tani 2.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako