• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yalegeza masharti dhidi ya kampuni ya akiba na mikopo

    (GMT+08:00) 2019-02-20 18:42:34

    Serikali ya Kenya imelegeza masharti ya utendaji kazi dhidi ya kampuni ya akiba na mikopo ya Ekeza ambayo humilikiwa na mshauri wa masuala ya kiuchumi nchini Kenya David Kariuki. Kwa mujibu wa Wizara ya Biashara, Viwanda na Vyama vya Ushirika, Ekeza sasa itakubaliwa kurejelea biashara zake japo kwa masharti kuwa ni lazima dili zake zote za kifedha ziwe zikiidhinishwa na serikali.

    Hii ni baada ya miaka miwili ya kuwekewa masharti ya kileseni ambapo Ekeza haijakuwa na uwezo wa kuhudumu kama kampuni ya uwekezaji.

    Mnamo Desemba 17, 2018, Kamishna wa Vyama vya Ushirika, Bi Mary Mungai aliunda kamati ya kuchunguza muundo wa kibiashara wa Ekeza kwa nia ya kuafikia maamuzi ya kurejeshewa au kunyimwa leseni.

    Ni katika hali hiyo ambapo Bi Mungai amethibitisha kuwa Alhamisi ijayo kutaandaliwa mkutano wa serikali na wanahisa wa Ekeza ili kuwapa ripoti ya uchunguzi na mapendekezo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako