Waziri wa Madini nchini Tanzania Bw Dotto Biteko ameagiza kusimamishwa kazi na kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa watumishi watano wa wizara hiyo kwa kukiuka vifungu vya Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Marekebisho yake ya Mwaka 2017.
Akizungumza mjini Dodoma, Biteko alisema watumishi watatu wamekiuka kifungu cha 16 cha Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya Mwaka 2017. Alisema kifungu hicho kinakataza maeneo yaliyoainishwa na kutangazwa na Serikali kwa wachimbaji wadogo yasitolewe leseni za uchimbaji wa kati wala mkubwa ili kuendeleza na kuwaimarisha kiuchumi wachimbaji wadogo. Alisema watumishi hao walihusika kugawa leseni za eneo la wachimbaji wadogo la Malela mkoani Morogoro bila kufuata utaratibu wa utoaji leseni katika maeneo hayo kwa mujibu wa kanuni ya 17 (3) ya Kanuni za Madini za Mwaka 2018.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |