• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yapaa Kenya ikichechemea

    (GMT+08:00) 2019-02-20 18:45:35

    Kenya iko katika hatari ya kupoteza nafasi yake kama simba wa uchumi Afrika Mashariki baada ya mataifa jirani hasa Uganda kufanikiwa kuuza bidhaa zaidi nyingi hapa nchini kuliko inazonunua.

    Hii inamaanisha kudidimia kwa viwanda vya Kenya, watu zaidi kupoteza nafasi za kazi na kupotea kwa ushuru.

    Ingawa Rais Museveni anasema Uganda imefanikiwa kuafikia haya kutokana na amani iliyoletwa na jeshi la nchi hiyo, wadadisi wanasema mazingara bora ya kiuchumi nchini humo ndiyo yamechangia hali hiyo.

    Takwimu zinaonyesha kuwa Wakenya wanaendelea kununua bidhaa kwa wingi kutoka mataifa jirani hasa Uganda na Tanzania badala ya kununua zinazotengenezewa nchini Kenya au zinazoigizwa nchini moja kwa moja kutoka ng'ambo kama vile India na China. Kwa kipindi cha miaka minne sasa, Uganda, ambayo haina bandari kama Kenya, imekuwa ikiuzia Kenya bidhaa za mabilioni ya pesa kuliko inazonunua hapa nchini. Bidhaa hizo ni pamoja na zinazotoka ndani ya uchumi wa Uganda kama vile mayai, maziwa, sukari na maharagwe. Pia wafanyibiashara wa Kenya wanasafiri Uganda kununua nguo, bidhaa za urembo, mbao na vipuri vya magari kwa ajili ya kuziuza nchini. Haya yote yametokana na serikali ya Kenya kuongeza ushuru wa bidhaa za humu nchini na zile za kutoka nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako