• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wazanzibar waonywa kuhusu utakatishaji wa fedha haramu

    (GMT+08:00) 2019-02-20 18:45:51

    Jaji mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu amesema utakatishaji wa fedha haramu una athari kubwa katika uchumi wa nchi na kwamba mapambano dhidi ya tatizo hilo hayataweza kufanikiwa iwapo jamii haitakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vyenye mamlaka husika. Jaji Makungu alisema utakatishaji wa fedha haramu una madhara makubwa ikiwamo kushusha uchumi hasa kwa mataifa yanayoendelea. Jaji Makungu alisema hayo wakati akifungua mafunzo ya siku mbili ya kuwajengea uwezo majaji, mahakimu na makadhi wa Zanzibar juu ya namna ya kushughulikia masuala ya fedha haramu. Alisema vitendo vya uhalifu na dawa za kulevya ambavyo ni miongoni mwa mambo yanayofanya utakatishaji wa fedha haramu vimekuwa vikidhibitiwa na kupungua kwa kiasi kikubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako