• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ongezeko la biashara duniani kuendelea kupungua katika robo ya kwanza ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-02-20 18:46:45

    Shirika la Biashara Duniani (WTO) limetoa ripoti mpya kuhusu hali ya biashara duniani na kusema, kama hali ya wasiwasi ya biashara haiwezi kutulia, kiasi cha ongezeko la biashara duniani katika robo ya kwanza ya mwaka huu kitaendelea kupungua.

    Ripoti hiyo iliyotolewa jana imeonesha kuwa, kielelezo cha ustawi wa biashara duniani katika miezi mitatu ya mwanzo ya mwaka huu kilipungua hadi 96.3 ambacho ni chini kabisa tangu mwezi Machi mwaka 2010.

    Kutokana na hali ya wasiwasi ya biashara duniani na kwa sera ya kupunguza utoaji wa fedha katika nchi zilizoendelea, mwezi Septemba mwaka jana WTO ilipunguza makadirio ya ongezeko la biashara ya bidhaa duniani katika mwaka 2018 na mwaka 2019 hadi asilimia 3.9 na asilimia 3.7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako