• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa pamba Kerio Valley wasaini na kampuni ya nguo

    (GMT+08:00) 2019-02-25 20:01:25

    Wakulima wa pamba katika bonde la Kerio wamesaini makubaliano na kampuni ya nguo ya Rivatex ya kuuza bidhaa hiyo kwa kampini hiyo.

    Awali wakulima hao walikuwa wamekosa soko la pamba na mara kwa mara walilaghaiwa na madalali wanaonunua kwa bei ya chini.

    Kulingana na makubaliano hayo, Rivatex itawapa wakulima hao mbegu na baadaye kununua mazao yao.

    Mwenyekiti wa wapanzi wa pamba kwenye neo hilo Peter Barngetuny, amesema wakulima wengi walikuwa wameacha kulima pamba kutokana na ukosefu wa soko.

    Naye naibu Gavana wa Elgeyo Marakwet Wisley Rotich amesema makubaliano hayo mapya yatawafaidi zaidi ya wakulima 1,000.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako