• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya nchi za kiarabu na Umoja wa Ulaya zaimarisha ushirikiano ili kukabiliana na changamoto

    (GMT+08:00) 2019-02-26 19:11:53

    Mkutano wa kwanza wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu na Umoja wa Ualya umefungwa huko Sharm el Sheikh, nchini Misri, na kuhudhuriwa na viongozi zaidi ya 50 kutoka nchi za kiarabu na za Ulaya. Mafanikio yaliyopatikana kwenye mkutano huo yameonesha kuwa taasisi hizo mbili kubwa za kikanda zina makubaliano mengi zaidi ya pamoja kuliko tofauti.

    Kuinuliwa kwa kiwango cha ushirikiano kati ya jumuiya ya nchi za kiarabu na Umoja wa Ulaya kunahusiana na hali ya kanda hizo mbili. Kwanza, hali ya usalama ni ngumu sana. Mashambulizi ya kigaidi yanatokea mara nyingi barani Ulaya, taasisi hizo mbili zinaona chanzo cha mashambulizi hayo ni wimbi kubwa la wakimbizi. Ili kutatua suala hilo, jumuiya ya nchi za kiarabu na Umoja wa Ulaya zinatakiwa kufanya juhudi kuchukua hatua halisi kupambana na uhamiaji haramu. Pili, kutokana na hali ya usalama, Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya na bei ya chini ya mafuta, hali ya uchumi ya kanda hizo mbili inaendelea kudidimia. Kujitoa kwa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya pia kutapunguza utegemezi wa kiuchumi wa nchi za kiarabu kwa Ulaya. Mbali na hayo, katika masuala ya Palestina na Israel, Syria, Libya na Yemen, nchi za kiarabu zinahitaji uungaji mkono wa Ulaya, hasa baada ya Marekani kuhamisha ubalozi wake nchini Israel kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem, msimamo wa Ulaya juu ya suala la Palestina na Israel ni muhimu sana. Umaalumu, ugumu na dharura ya hali ya kanda hizo zimefanikisha mkutano huo.

    Kutokana na maazimio ya mkutano wa kilele wa Sharm el Sheikh, mafanikio ya ushirikiano kati ya pande mbili yamekuwa mazuri zaidi kuliko matarajio. Ingawa nchi za Umoja wa Ulaya zimekuwa na migongano katika mgao wa wakimbizi, lakini maazimio hayo yameonesha kuwa pande mbalimbali zimefikia makubaliano kuhusu uhamiaji haramu na suala la wakimbizi. Katika mkutano huo, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imeungwa mkono na nchi za Umoja wa Ulaya katika masuala ya Palestina na Israel, Syria na Libya. Hasa Umoja wa Ulaya umekubali kuhakikisha hadhi ya Jerusalem, huku ukisisitiza tena kuhimiza kutatua suala la Palestina kwa kufuata azimio husika la Umoja wa Mataifa. Lakini taasisi hizo mbili hazijafikia makubaliano yoyote juu ya suala la uchumi na biashara. Hii inamaanisha kuwa, pande hizo mbili bado zina wasiwasi juu ya mustakabali wa ushirikiano wa kikanda baada ya Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako