• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Upungufu wa viatilifu wawaliza wakulima wa Pamba Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-02-26 20:26:40

    Wakulima wa pamba ,nchini Tanzania wana hofu ya kupata mavuno kidogo na kushuka kiuchumi kutokana na upungufu wa viatilifu vya kuulia wadudu wanaoshambulia zao hilo mashambani.

    Hayo yalisema jana na Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Geita,Zainabu Mahenge ,kwenye kikao cha wadau wa zao la pamba mkoani Shinyanga,chenye lengo la kuimarisha kilimo cha zao hilo.

    Alisema wakulima mkoani Shinyanga wamelima kwa wingi zao hilo ,lakini changamoto ni kuwapo na upungufu wa viatilifu na baadhi ya mashamba yao yameanza kushambuliwa na wadudu na kukatishwa tama kuendelea na kilimo cha zao hilo.

    Aidha Mahenge alitoa rai kwa Bodi ya Pamba kama imeshindwa kusambaza viatilifu hivyo vya kuulia wadudu kwa wakulima,itoa zabuni kwa kampuni nyingine ambayo itakuwa na uwezo wa kuvisambaza haraka kwa wakulima,na vya kutosha.

    Meneja wa Bodi ya Pamba kutoka kanda ya Ziwa ,Jones Bwahama,alikiri kuwapo na upungufu huo wa viatilifu vya kuulia wadudu na kubainisha kuwa serikali sasa ishaanza kuvisambaza kwenye mikoa mbalimbali kwa usafiri wa ndege ili kuhakikisha zao hilo halipotei.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako