• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zama ya 5G itakayowadia yahitaji ufunguaji mlango na ushirikiano wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-02-27 19:14:30

    Hili ni suala linalojadiliwa zaidi kwenye Mkutano wa mawasiliano ya simu duniani unaofanyika mjini Barcelona, Hispania, ni ujio wa zama ya 5G, ambayo ni ishara wazi inayooneshwa kutoka mkutano huo kwa dunia nzima.

    Kwenye mkutano huo wenye kauli mbiu ya "kuunganishwa kwa njia ya akili bandia", kampuni kubwa za mawasiliano ya simu duniani zimeonesha teknolojia na bidhaa zao za kisasa, ikiwemo teknolojia na bidhaa za 5G, hali ambayo inawafanya watu wagundue kuwa mlango wa zama ya 5G utafunguliwa.

    Teknolojia ya 5G itaweza kutumiwa katika maisha ya kawaida, kwa mfano madaktari wataweza kufanya upasuaji kwa umbali mkubwa kupitia mtandao wa internet wa 5G; mfumo wa kutokuwa na dereva unaweza kupunguza kasi ya kusimamisha gari linaloendeshwa kutoka sekonde 0.4 hadi sekonde 0.001; na watumiaji wa simu za mikononi wataweza kutazama video kwa urahisi zaidi.

    Ingawa vigezo vyote vinavyohusu mtandao wa 5G vitapitishwa kwa pande zote kwenye Shirikisho la Kimataifa la Mawasiliano ya Simu mwaka 2020, lakini kampuni mbalimbali zimeonesha simu au teknolojia za 5G kwenye mkutano huo, na kampuni za China zinafuatiliwa zaidi. Kwa mfano, Mate X ya Kampuni ya Huawei ambazo skrini yake inaweza kufungwa na kufunguliwa, na inatajwa kama ni "simu kutoka siku za baadaye". Hata hivyo, njia ya 5G ya kuelekea kwenye zama mpya bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

    Zama ya 5G inahitaji ushirikiano wa kimataifa katika maeneo mengi. Hivi sasa nchi na sehemu nyingi duniani bado zinatumia teknolojia za 2G, 3G, na 4G, na zitakabiliwa na matatizo mbalimbali katika kufikia ngazi ya 5G. Ni hadi nchi mbalimbali zitakapofanya ushirikiano mpana zaidi, ndipo zitakapoweza kukabiliana na changamoto hizo na kuwanufaisha watu kwa njia ya 5G. Hivi sasa kampuni nyingi za China zikiwemo Huawei zimesaini makubaliano na kampuni zaidi ya 30 za kimataifa, na vituo zaidi ya elfu 40 vya 5G vimeuzwa kote duniani. Kampuni ya ZTE pia imeanzisha ushirikiano na kampuni zaidi ya 30 duniani.

    Mhandisi mkuu wa Wizara ya viwanda na TEHAMA ya China Bw. Zhang Feng ametoa wito kwa kampuni mbalimbali za mawasiliano ya simu duniani kushirikiana katika kulinda mazingira ya maendeleo ya sekta hiyo yaliyo na usawa, haki na uwazi, ili kuhimiza ushindani wa sekta hiyo ifuate kanuni za soko na kimataifa, na kuyafanya mapinduzi ya teknolojia mpya ikiwemo 5G kuunganisha nchi na watu wa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako