• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zanzibar: Zanzibar inatarajia kujenga uwanja wa ndege wa kisasa

  (GMT+08:00) 2019-02-27 19:51:38

  Serikali ya Zanzibar, inatarajia kujenga uwanja wa ndege wa kisasa kisiwani Pemba utakaoruhusu kutua ndege kubwa.

  Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, aliyasema hayo, wakati wa majumuisho ya ziara yake kisiwani humo.

  Alisema kuwa uwanja huo utakuwa wa kisasa na mkubwa utakaoruhusu ndege za aina zote kubwa kutua katika kiwanja hicho na kusaidia usafiri wa anga.

  Alisema tayari mchakato wake umeanza na ameshatuma mawaziri 10 kwenda kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya ujenzi ili wakae tayari ujenzi utakapoanza waweze kuondoka katika eneo hilo na kupewa fedha kwa ajili ya mali zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako