• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magongo: Butali wafalme Parklands Open

    (GMT+08:00) 2019-02-28 08:10:46
    Wafalme wa magongo nchini Kenya Butali Warriors wamejitahidi kiume na kutawazwa mabingwa wa shindano la Parklands Open katika uwanja wa Parklands jijini Nairobi.

    Butali ya kocha Dennis Owoka imebeba taji hilo baada ya kuwashinda Wazalendo mabao 2-1 katika mchezo wa fainali ya kusisimua.

    Klabu ya Butali inayojivunia kusajili wachezaji kadhaa kujiandalia msimu mpya wa Ligi Kuu, ilivuna ufanisi huo kupitia mabao ya sajili mpya Calvin Kanu na Moses Ademba naye Dennis Mwanzo aliipatia Wazalendo bao la kufuta machozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako