• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zoezi la kukusanya picha kuhusu pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" laanzishwa

  (GMT+08:00) 2019-02-28 15:32:56

  Zoezi la kukusanya picha kuhusu pendekezo la "'Ukanda Mmoja, Njia Moja' kupitia kamera yako" linaloandaliwa na Tovuti ya Mtandao wa Internet ya CRI Online, limeanza rasmi. Sasa CRI Online inapanga kukusanya picha kutoka kwa watumiaji wote wa mtandao wa Internet duniani kwa kupitia vyombo vipya vya habari kwa kutumia lugha mbalimbali, mitandao ya kijamii nchini China na nchi za nje, pamoja na vyombo vya habari vya kiubia katika nchi za nje.

  Shughuli hiyo inalenga kuonesha maendeleo yaliyopatikana katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na moyo wa "Njia ya Hariri" unaofuata msingi wa "kufanya ushirikiano kwa njia ya amani, kufungua mlango na shirikishi, kusaidiana na kunufaishana, pia kuonesha mabadiliko na sura mpya yanayoletwa kutokana na pendekezo hilo, na kurekodi mawasiliano ya kirafiki, utamaduni na urafiki kati ya wachina na nchi zilizojiunga na pendekezo hilo, pia kuonesha mila na desturi za nchi husika.

  Shughuli hiyo itafanyika kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe 10 Aprili, ambapo kuanzia tarehe 28 Februari hadi tarehe 28 Machi ni kipindi cha kukusanya picha. Kuanzia tarehe 29 Machi hadi tarehe 9 Aprili utafanyika ukaguzi wa hatua ya mwanzo, na matokeo yatatangazwa rasmi tarehe 10 Aprili.

  Wakati wa shughuli hiyo, watumiaji wa mtandao wa internet kutoka nchi mbalimbali wataweza kututumia picha kwa parua pepe (E-mail: withyou2019@qq.com), au kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook @ kiswahilicri. Kanuni halisi za shughuli hiyo zimewekwa kupitia www. cri.cn/withyou.

  Turekodi njia ya kupata maendeleo kwa pamoja kupitia picha. Kamera yako itashuhudia historia ya mawasiliano ya kirafiki ya binadamu katika karne ya 21!

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako