• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Kagame aitaka Afrika kufungua anga

    (GMT+08:00) 2019-02-28 19:43:23

    Rais wa Rwanda Paul Kagame amezitaka nchi za Afrika kufungua anga zao ili kurahisisha uchukuzi wa anga na kukuza sekta ya uchukuzi huo barani humo.

    Kagame amezungumza kwenye mkutano wa siku mbili wa wadau wa sekta ya uchukuzi wa anga mjini Kigali Rwanda.

    Amesema utekelezaji wa Soko la Usafiri wa Ndege wa Afrika utasaidia kuondoa changamoto za kijiografia ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa ukuaji wa sekta hiyo.

    Hadi sasa ni nchi 28 tu barani Afrika ambazo zimefungua anga zao na inasalia kuwa vigumu kuhudumu katika baadhi ya nchi kwani hazijatoa idhhini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako