• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Portalnd yangaza hasara zaidi

    (GMT+08:00) 2019-02-28 19:45:46

    Kampuni ya saruji ya Portland nchini Kenya imetangaza hasara ya shilingi bilioni 1.2 katika kipindi kilichokamilika disemba mwaka 2018.

    Kulingana na ripoti ya kifedha iliotolewa na kampuni hiyo, kufilisika kwake kuliongezeka kwa shilingi bilioni 1.3 katika miezi sita tu.

    Kipindi sawa na hicho mwaka jana kampuni hiyo ilipata hasara ya shilingi milioni 969.

    Katibu wa kampuni hiyo Sheila Kahuki amesema kupanda kwa gharama za oparesheni na kudhoofika kwa soko kumechangia hasara hiyo kubwa.

    Kwa sasa kampuni hiyo inakabiliwa na deni la shilingi bilioni 10 kiasi kikubwa kikidaiwa na benki ya KCB cha bilioni 4.5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako