• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wafugaji nyandarua walalamikia kushuka kwa bei ya maziwa

    (GMT+08:00) 2019-02-28 19:46:02

    Wafugaji wa ng'ombe wa maziwa katika kaunti ya Nyandarua nchini Kenya wamelalamikia kupunguzwa kwa bei ya bidhaa hiyo.

    Sasa lita moja inauzwa kwa shilingi 25 ikilinganishwa na ile ya awali ya shilingi 30.

    Wakulima wanalaamika kuwa kampuni za maziwa kwenye kaunti hiyo zimepunguza bei licha ya kuwa mahitaji ya bidhaa hiyo yamepanda.'

    Viongozi kwenye eneo hilo hata hivyo wamelaumu madalali ambao wanawalaghai wakulima na kuitaka serikali kutafuta suluhu la haraka.

    Sasa wakulima wanasubiri mitambo 35 mipya ya kuhifadhia maziwa ilioahidiwa na naibu wa Rais William Ruto alipozuru eneo hilo.

    Wanasema kwa kuhifadhi maziwa wataweza kuthibiti bei wenyewe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako