• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Serikali ya Uganda yatoa shilingi bilioni 40 kuwafidia wafanyabiashara

    (GMT+08:00) 2019-02-28 19:46:20

    Serikali ya Uganda imetoa shilingi bilioni 40 kuwafidia watu na kampuni ambazo ziliwasilisha bidhaa zao nchini Sudan Kusini kabla ya nchi hiyo kutumbukia katika machafuko mwaka 2013.

    Hata hivyo sio wafanyabiashara wote watapata fidia hiyo.

    Mwenyekiti wa wafanyabishara wa mji mkuu Kampala Everest Kayondo, amesema watu waliowasilisha bidhaa zao kwa watu binafsi huenda wakasubiri kwa muda kabla ya kupayta fidia yao.

    Amesema hiyo inatokana na kuwa bado wizara ya biashara ya Uganda na ile ya Sudan Kusini hazikamilisha zoezi la uhakiki.

    Kayondo amesema kuwa changamoto kubwa ni baadhi ya wafanyabiashara kukosa stakabadhi muhimu kama vile risiti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako