• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wauzaji vipodozi waonywa Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-02-28 19:46:54

    Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Kanda ya Kati, imewaonya baadhi ya wafanyabiashara wa vipodozi wanaoendelea kukiuka sheria za dawa na vipodozi kwa kuuza vitu vilivyopigwa marufuku.

    Meneja wa mamlaka hiyo Kanda ya Kati, Dk. Englibert Bilashoboka, alisema TFDA inaendelea na misako ya kuwatafuta wanaokiuka sheria ili wachukuliwe hatua.

    Dk. Bilashoboka alisema wafanyabiashara hao wamekuwa wakishawishi wanawake wanaovitumia kwa ajili ya kubadilisha ngozi zao kutoka kuwa weusi kwenda kwenye weupe.

    Alivitaja baadhi ya vipodozi vilivyopigwa marufuku ni carolight, medvin na Tentclair na vinavyotokana na kemikali hatari zinazoitwa kama vile hydroquinone, mercury na steroids.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako