• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani wakutana kwa mara ya pili

    (GMT+08:00) 2019-02-28 21:26:47

    Kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un na rais Donald Trumps wa Marekani kwa nyakati tofauti wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na mazungumzo ya kikundi cha ujumbe mjini Hanoi, Vietnam, lakini mazungumzo yamemalizika mapema.

    Mkutano wao ulimalizika bila ya kusainiwa kwa nyakara za makubaliano kwa mujibu wa mpango uliowekwa. Ingawa makubaliano hayakufikiwa, lakini matokeo hayo labda si mabaya zaidi, labda hiyo ni sehemu moja ya juhudi za muda mrefu kwenye mchakato wa utatuzi wa suala la nyukilia la peninsula ya Korea.

    Kwanza, tangu mkutano wa kilele uliofanyika mwezi Juni huko Singapore, baada ya duru mbili za mazungumzo kati ya viongozi wa nchi hizo mbili, pande mbili hizo zimefikia maelewano mengi zaidi na kufahamu zaidi ufuatiliaji na matarajio ya upande mwingine na kuweka msingi kwa majadiliano ya baadaye. Wakati huohuo, mkutano huo umegusa kiini cha ufuatiliaji wa pande mbili. Kwa mfano, Bw. Kim amesema kuwa kama hataki kuondoa silaha za nyuklia kwenye peninsula ya Korea, asingekwenda Hanoi, Vietnam. Habari zinasema, kwenye mkutano huo, upande wa Marekani ulipendekeza kufungua ofisi nchini DPRK, na pandekezo hilo limepata jibu la upande mwingine.

    Suala la nyuklia la Korea Kaskazini limedumu kwa miongo kadhaa, na halitaweza kutatuliwa kabisa kupitia mikutano michache ya viongozi, na kukosa uaminifu katika miaka mingi iliyopita pia hakuwezi kuondolewa kabisa ndani ya muda mfupi. Matokeo yaliyopatikana kwenye mazungumzo hayo pia yameonesha utatanishi wa suala hilo.

    Kutokana na mchakato wa mabadiliko ya uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Marekani, ni wazi kuwa mazungumzo ni njia sahihi na ya kipekee kwa kutatua suala la nyuklia la Peninsula ya Korea. Kama waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi alivyosema wakati alipokutana na naibu waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini Bw. Ri Kil-Song, mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Marekani yamehusisha masuala ya kina, ndiyo maana yanakabiliwa na matatizo mbalimbali. Bw. Wang Yi amesema China inatarajia nchi hizo mbili zitaimarisha uaminifu kati yao, kudumisha uvumilivu, kuendelea na mazungumzo, kufanya juhudi za kusaidiana, na kufanya jitihada za kutosha kutimiza malengo yaliyowekwa. Amesema China pia ina nia ya kuendelea kufanya jukumu la kiujenzi katika suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako