• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • VOLIBOLI: Agala akabidhiwa unahodha tayari kwa michuano ya klabu bingwa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-03-01 08:37:42
    Brackcides Agala amekabidhiwa unahodha wa kikosi cha Kenya Prisons kitakachowania ubingwa wa klabu bingwa barani Afrika (CAVB) kwa voliboli ya wanawake itakayofanyika mwezi huu jijini Cairo, Misri.

    Agala anatwaa unahodha kutoka kwa mshambuliaji Evelyne Makuto aliyewaongoza Prisons kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya voliboli (KVF) mwishoni mwa msimu uliopita.

    Kocha wa timu hiyo Josp Barasa amesema kikosi chake kiko imara na tayari kwa mashindano hayo, na kuahidi kufanya vizuri na kuzoa mataji mengi zaidi msimu huu hususani katika ulingo wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako