• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: AFCON 2019: Timu ya taifa ya Burundi yaita wachezaji wake kuingia kambini

  (GMT+08:00) 2019-03-01 08:40:11

  Benchi la ufundi la timu ya taifa ya Burundi chini ya kocha wake mkuu Olivier Niyungeko limeita wachezaji 23 ikiwemo wanaokipiga nje ya nchi kwa ajili ya kuingia kambini kujiandaa kwa mchezo dhidi ya Gabon utakaopigwa Machi 22 mjini Bujumbura.

  Burundi inahitaji ushindi ama sare yeyote kwenye mchezo huo wa kundi C ili kujihakikishia tiketi ya kufuzu kombe la mataifa ya Afrika baadaye mwaka huu.

  Wachezaji Amis Tambwe anayechezea timu ya Yanga na mwenzake Blaise Birigimana wanaokipiga nchini Tanzania hawajaitwa katika kikosi hicho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako