• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Francis Kimanzi ashinda tuzo ya kocha bora nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2019-03-01 08:38:38
    Kocha mkuu wa klabu ya Mathare United FC inayoshiriki ligi kuu ya Kenya ya SportPesa (KFC) Francis Kimanzi, ametangazwa mshindi wa Tuzo ya kocha bora wa mwezi januari mwaka huu.

    Kimanzi, amewashinda makocha wengine Bernard Mwalala wa Bandari FC na Hassan Oktay wa Gor Mahia, ambao pia walikuwa wanawania tuzo hiyo.

    Hii ni mara ya tatu kwa Kimanzi, alikuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, kushinda tuzo hiyo. Mkufunzi huyo pia alishinda tuzo ya kwanza ya kocha bora iliyoanzishwa mwezi machi mwaka 2016 kabla ya kushinda tena tuzo ya pili ya mwezi machi uliofuatia 2017.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako