• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nairobi Water Queens mabingwa ligi ya taifa

    (GMT+08:00) 2019-03-04 11:47:00
    Nairobi Water Queens wametangazwa mabingwa kwa mara ya pili mfululizo taji la ubingwa wa ligi ya taifa katika mchezo wa mpira wa Mikono (Handiboli) kwa wanawake msimu huu nchini Kenya.

    Klabu hiyo imefanikiwa kunyanyua taji hilo kwa kumaliza wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na jumla ya alama 32 na kumaliza msimu wa ligi hiyo, iliyoshirikisha timu tisa za wanawake, bila kupoteza mechi hata moja.

    Kutokana na ubingwa huo, timu hiyo wamekata tiketi ya kuiwakilisha Kenya kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika itakayofanyika Oktoba mwaka huu nchini Morocco.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako