• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Maombi ya kusamehewa kodi yakataliwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-03-04 19:03:37
    Maombi 130 ya walioomba kusamehewa riba ya kodi ya malimbikizo kwa walipa kodi mbalimbali nchini Tanzania, yamekataliwa kutokana na kutokidhi vigezo vya kusamehewa.

    Aidha, walipakodi hao kwa sasa watatakiwa kulipa kiasi walichokuwa wanadaiwa ikiwamo riba na faini, kwa mujibu wa sheria.

    Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema maombi yaliyowasilishwa ni 9,220 na yaliyokubaliwa ni 6,987.

    Julai, mwaka jana, TRA ilitangaza vigezo sita kwa wanaostahili kupata msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya kodi na kupewa siku 30 za kukamilisha malipo hayo.

    Alisema maombi 2,113 yalikuwa chini ya ukaguzi maalum ili kujiridhisha nayo kabla ya utekelezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako