• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Malawi: Uzalishaji wa mahindi kuongezeka Malawi

    (GMT+08:00) 2019-03-04 19:03:55
    Malawi inatarajia kuongeza uzalishaji wake wa mahindi kwa zaidi ya asilimia 20 katika msimu huu.

    Wizara ya kilimo nchini humo inatarajia kuwa uzalishaji utafikia tani milioni 3.4 ikilinganishwa na tani milioni 2.6 za mwaka uliopita.

    Waziri wa kilimo Joseph Mwanamvekha amesema ongezeko hilo linatokana na mvua za kutosha ambazo zimenyesha kwa usawa karibu maeneo yote na pia mipango ya serikali ya kuwekeza kwenye uzalishaji wa chakula.

    Mwanamvekha amesema serikali imetoa mbegu aina ya maharage za ekari 3,900 na zaidi ya lita 25,000 za dawa za kupambana na wadudu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako