• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kupunguza kodi zaidi

    (GMT+08:00) 2019-03-05 16:35:04

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang ameahadi kuwa mwaka huu serikali ya China itapunguza kodi kwa kiasi kikubwa zaidi, hasa kozi za sekta ya utengenezaji na kampuni ndogondogo.

    Hayo yamo kwenye ripoti ya kazi za serikali iliyotolewa leo na Bw. Li Keqiang. Ripoti hiyo imesema, kodi ya asilimia 16 ya sekta ya utengenezaji itapungua hadi asilimia 13, na kodi ya sekta za uchukuzi na ujenzi itapungua hadi asilimia 9.

    Ili kupunguza mizigo kwa kampuni , ripoti hiyo pia inasema mwaka huu serikali ya China itapunguza gharama za matumizi ya umeme ya sekta ya utengenezaji, na kuondoa kimsingi vituo vya kulipa fedha vya mipaka ya mikoa ndani ya miaka miwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako