• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuweka mkazo katika kuboresha mazingira ya maendeleo ya sekta binafsi

    (GMT+08:00) 2019-03-05 16:36:37

    Ripoti ya kazi ya serikali iliyowasilishwa leo na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang kwenye mkutano wa Bunge la umma la China inasema, China itaweka mkazo katika kuboresha mazingira ya maendeleo ya sekta binafsi, kuhamasisha, kuunga mkono na kuelekeza maendeleo ya sekta hizo, na kuyatendea mashirika yote ya kichumi kwa usawa.

    Ripoti hiyo inasema, China inapanga kujenga uhusiano mpya kati ya serikali na mashirika ya kibiashara, kukamilisha utaratibu wa mawasiliano kati ya pande mbili, kuhamasisha ujasiriamali, na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa sekta binafsi.

    Ripoti pia imesisitiza dhamira ya China ya kulinda hakimiliki na kutoa adhabu dhidi ya vitendo vyovyote vinavyokiuka hakimiliki kwa mujibu wa sheria, ili kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako