• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapendekeza kutatua mgogoro wa biashara kwa mazungumzo ya usawa

    (GMT+08:00) 2019-03-05 16:38:49

    Ripoti ya kazi ya serikali ya China inayowasilishwa leo kwenye mkutano wa bunge la umma la China inasema, China inapendekeza kutatua mgogoro wa biashara kwa mazungumzo ya usawa, na inatekeleza ahadi yake kwa makini, na kulinda kithabiti haki zake halali.

    Ripoti hiyo imesisitiza kuwa, China inalinda kithabiti mafungamano ya kiuchumi na biashara huria. Katika mwaka huu, China itaharakisha kujenga mtandao wa eneo la biashara huria wenye kigezo cha ngazi ya juu, kuhimiza makubaliano ya uhusiano wa kiwenzi ya uchumi wa kikanda. Pia kuanzisha eneo la biashara huria kati ya China, Japan na Korea Kusini, kuendelea na mazungumzo ya makubaliano ya uwekezaji kati ya China na Ulaya, na kuendelea kuhimiza mazungumzo ya kibiashara kati ya China na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako