• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyabiashara wa Uganda na Rwanda kufuatia kufungwa kwa mpaka

    (GMT+08:00) 2019-03-05 18:50:17

    Serikali za Uganda na Rwanda ziliendelea kulaumiana kuhusu mzozo uliosababisha mpaka wa nchi hizo mbili kufungwa na kuwafanya wafanyabiashara wa pande zote mbili kupata hasara .

    Taharuki ilitanda Jumatano iliyopita wakati magari yote ya mizigo kutoka Uganda yalipokatazwa kuingia Rwanda kupitia mpaka wa Katuna-Gatuna.

    Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Rwanda, Richard Sezibera alisema ingawa "hakuna mtu anakatazwa kusafiri hadi Uganda," Wanyarwanda wameshauriwa dhidi ya kwenda katika nchi hiyo kwa ajili ya usalama wao wenyewe. Mnamo Alhamisi, mamia ya wasafiri walikwama katika mpaka wa nchi hizo mbili baada ya maafisa wa uhamiaji kuwazuia kuingia Uganda.

    Baadhi ya wasafiri ambao wengi wao ni wafanya biashara walijaribu kuewasihi maafisa wa mpakani lakini hawakusikilizwa. Madereva wa malori waliohojiwa walisema hawakujulishwa kuhusu mpango wa kufunga mpaka huo na hivyo wakapata hasara kubwa. Biashara ziliathirika pakubwa kwani mizigo haingevukishwa mpakani na pia wafanyabiashara wadogo walikosa mbinu ya kusafirisha mizigo yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako