• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kituo cha kusambaza umeme Kigamboni chakamilika

    (GMT+08:00) 2019-03-05 18:50:36

    Hatimaye kilio cha wakazi wa Kigamboni nchini Tanzania kuhusu uhaba wa umeme kimepatiwa ufumbuzi baada ya kukamilika kwa kituo kidogo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini.

    Kituo hicho kilichojengwa kwa ajili ya kusambaza umeme Kigamboni kinatarajiwa kuzalisha megawati 20 kuanza Machi 6.

    Kupatikana kwa megawati hizo kutaongeza kiwango cha umeme kwa wilaya hiyo kufikia megawati 37 zikijumuishwa na 17 zinazopatikana sasa.

    Akizungumza baada ya kutembelea kituo hicho jana, katibu mkuu wizara ya nishati, Dk Hamis Mwinyimvua alisema kuanza kazi kwa kituo hicho kutaondoa kero kwa wakazi wa wilaya hiyo ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia umeme.

    Naye meneja wa Tanesco Kigamboni, mhandisi Khadija Abdallahmed alisema kuanza kufanya kazi kwa kituo hicho kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa malalamiko ya wakazi wa Kigamboni kuhusu adha ya umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako