• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa Kenya kuwa imara mwaka huu

    (GMT+08:00) 2019-03-05 18:50:59

    Wachambuzi wa mambo ya uchumi nchini Kenya wamesema uchumi wa Kenya mwaka huu utashuhudia ukuaji wa asilimia 5.8 ikiwa ni juu kuliko mwaka jana kufuatia uwekezaji kutoka kwa sekta ya kibinafsi.

    Wachambuzi hao wamesema mafanikio hayo yamechangiwa na mvua kubwa iliyonyesha katika robo ya pili mwaka jana pamoja na salamu za maridhiano ya kisiasa kati ya rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga. Wachambuzi hao wamesema maisha ya wakenya yataimarika huku nafasi za ajira zikiongezeka kufuatia kuongezeka kwa miradi mingi ya miundo mbinu kama vile barabara na reli.Serikali ya Uhuru Kenyatta imepongezwa sana kutokana na kuanzisha miradi mingi ambayo imechangia kupatikana kwa ajira kwa vijana na wakati huo huo kupiga jeki uchumi wa nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako