• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shirika la mazingira la UM lasema ujenzi wa ustaarabu wa kiikolojia wa China umepata maendeleo makubwa

    (GMT+08:00) 2019-03-06 09:43:30

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana kwenye ripoti kuhusu kazi za serikali, alisema mwaka jana China ilihimiza udhibiti wa uchafuzi kwa pande zote, na kujitahidi kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Shirika la mazingira ya Umoja wa Mataifa Bi. Joyce Msuya amesema,

    "Mkutano wa Pili wa Bunge la awamu ya 13 la Umma la China NPC unafanyika mjini Beijing, ambao unaweka mpango wa ustaarabu wa kiikolojia wa China katika siku za usoni. Nafurahi kuona kwamba serikali ya China inaendeleza kwa kina juhudi za kudhibiti uchafuzi na kuhimiza nishati endelevu."

    Ripoti hiyo pia imesema China inapaswa kuimarisha udhibiti wa uchafuzi na ujenzi wa kiikolojia, na kuhimiza maendeleo yasiyosababisha uchafuzi. Pia kuna haja ya kurekebisha kanuni husika, ili kuhimiza maendeleo yenye ubora na uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia. Bibi Msuya ameongeza kuwa China imethibitisha nguvu ya uongozi kuhusu udhibiti wa uchafuzi, na ana matumaini makubwa na juhudi za China katika uhifadhi wa mazingira. Amesema,

    "Niliwahi kukaa hapa Beijing tangu mwaka 2011 hadi 2014, ambapo niliwahi kushuhudia kazi ya uongozi iliyofanywa na serikali ya China katika kutatua suala la vumbi la PM 2.5. China ni nchi kubwa yenye uanuwai wa kiikolojia, tumeona maendeleo makubwa yaliyopatikana hapa China. Tunatumai kuona mabadiliko zaidi katika siku za usoni kama Bw Li Keqiang alivyotangaza leo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako