• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yasifu ripoti ya kazi ya serikali aliyoitoa waziri mkuu wa China

    (GMT+08:00) 2019-03-06 09:53:33

    Wachambuzi wa mambo ya siasa na biashara wa nchi za nje, wameanza kuchambua ripoti ya kazi iliyowasilishwa na waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang kwenye Mkutano wa Pili wa Bunge la awamu ya 13 la Umma la China.

    Wachambuzi hao wanaona mafanikio yaliyopatikana na China katika mwaka uliopita yanatokana na juhudi kubwa, na wanatarajia maendeleo hayo yatanufaisha zaidi dunia nzima.

    Bw. Li Keqiang amesema kwenye ripoti hiyo kuwa, China imetimiza malengo makuu ya maendeleo ya uchumi na jamii kwa mwaka uliopita kwa kufuata wazo la ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya, na kupata maendeleo makubwa katika kukamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora.

    Mkurugenzi Kituo cha utafiti wa mambo ya China cha Nigeria Bw. Charles Onunaiju amesema serikali ya China inatatua bila kusita matatizo mapya yanayoibuka, na anaamini kuwa itaweza kufikia matarajio ya wananchi kuhusu maisha bora, na kuzidi kuinua kiwango cha utamaduni na maisha ya wananchi. Amesema ripoti hiyo imeweka lengo la ongezeko la Pato la Ndani GDP kwa mwaka huu kuwa kati ya asilimia 6 na 6.5. Na kusema kwamba China itachukua hatua za kuhimiza nguvu ya soko la ndani, na kuendelea kupanua mahitaji ya ndani.

    Mkurugenzi wa Kituo cha utafiti cha kundi la vyombo vya habari la Peninsula ya Qatar Bw. Mohammed ameeleza kuwa, nchi mbalimbali duniani zinazingatia mabadiliko na marekebisho kuhusu sera ya uchumi wa China, na vitu vinavyosaidia maendeleo ya uchumi wa China vilevile vinachangia maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya mambo ya kimataifa ya Afrika Kusini Dk. Cobus Van Staden amesema, pendekezo la China la kuhimiza maendeleo yenye ubora ya viwanda vya utengenezaji bidhaa ni hatua ya kiuvumbuzi, ambalo litaihimiza sekta ya viwanda ya China ifikie kwenye ngazi ya juu zaidi.

    Naye Bw. Onunaiju akizungumzia ripoti ya kazi ya serikali inayosema kwamba, China ina nia thabiti na uwezo katika kukabiliana na matatizo mbalimbali, amesema ufunguaji mlango wa China utahakikisha China inajihusisha vizuri zaidi katika uchumi wa dunia nzima, hali ambayo itaongeza imani ya nchi nyingine katika kujiunga na pendekezo la uchumi la China, pia anaamini kuwa ustawi wa China utainufaisha dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako