• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema kujenga kigezo wazi cha usalama wa mtandao wa Internet ni pendekezo la kiujenzi

    (GMT+08:00) 2019-03-06 19:30:17

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema, China inapendekeza jumuiya ya kimataifa kushirikiana kukabiliana tishio la usalama wa mtandao wa Internet kwa kupitia mazungumzo na ushirikiano, juu ya msingi wa kuheshimiana na kunufaishana.

    Bw. Lu Kang amesema, usalama wa mtandao wa Internet ni suala la dunia nzima, unahusiana na maslahi ya pamoja ya nchi mbalimbali, na unapaswa kulindwa kwa pamoja na jumuiya ya kimataifa. China inaona kuwa, kujenga kigezo cha pamoja na cha wazi cha usalama wa mtandao wa Internet ni pendekezo la kiujenzi.

    Hivi karibuni, waziri mkuu wa Ureno Bw. Antonio Costa alisema nchi za Umoja wa Ulaya hazipaswi kutumia vibaya ukaguzi wa usalama ili kubagua uwekezaji kutoka nje ya umoja huo. Alisema Ureno inaelewa wasiwasi wa baadhi ya nchi kuhusu hatari inayotokana na kushiriki kwenye mtandao wa 5G wa Huawei, lakini hazipaswi kusitisha mchakato wa utandawazi wa kisasa wa miundo mbinu ya kidijitali ya Ulaya.

    Aidha, kituo cha usalama wa wazi wa mtandao wa Internet cha Huawei kimezinduliwa jana mjini Brussels, na kampuni hiyo imetoa mwito kwa nchi husika kujenga kigezo cha pamoja na cha wazi cha usalama wa mtandao wa Internet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako