• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wauzaji kahawa Uganda wapanga kuacha kuuza bidhaa hiyo kupitia soko la mnada la Mombasa

    (GMT+08:00) 2019-03-06 20:02:52

    Wasindikaji wa kahawa nchini Uganda wanataka kuacha kuuza kahawa yao kupitia masoko ya mnada kama vile Mombasa,wakisema kuwa wanataka kuanza kuuzia moja kwa moja wanunuzi.

    Uganda inauza chai,kahawa,miongoni mwa bidhaa nyengine kupitia Mombasa.

    Akizungumza na maafisa kutoka Shirika la Trademark East Afrika katika ofisi za Mamlaka ya Maendeleo mjini Lugogo jana,Meneja wa Chama cha Ushirika cha Ankole ,Bw John Nuwagaba alisema kuuza moja kwa moja sokoni ni vyema kuliko kuuza kupitia kwenye soko la mnada.

    Kulingana na Benki Kuu ya Uganda,Uganda ilisafirisha magunia 4.1milioni (60kg) ya kahawa katika kipindi cha mwaka ulioisha 2018,na kuingiza zaidi ya $436m .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako