• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa fedha wa China asema kupunguza kodi kutapewa kipaumbele katika sera ya mambo ya fedha

    (GMT+08:00) 2019-03-07 16:55:26

    Waziri wa fedha wa China Bw. Liu Kun leo amesema, sera ya mambo ya fedha ya China itaimarishwa, na wakati inapopunguza kodi, China itapanua matumizi ya fedha na kuongeza nguvu za kutenga fedha katika sekta muhimu na mambo muhimu.

    Bw. Liu Kun amesema, China itapunguza kodi na ada kwa kiasi kikubwa, kuongoza makampuni kuwa na matarajio mwafaka na kuimarisha imani ya soko, na kutuliza maendeleo ya uchumi. Vilevile kuzidisha mageuzi ya kodi ya VAT kutakuwa mambo muhimu ya kupunguza kodi na ada ya mwaka huu.

    "Kupunguza kodi ya makampuni ya utengenezaji hadi asilimia 13 kutoka asilimia 16, kupunguza kodi ya sekta za usafirishaji na ujenzi hadi asilimia 9 kutoka 10, kuhakikisha kodi za sekta muhimu kupunguzwa kwa dhahiri. Tutachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kodi za sekta zote zinapunguzwa."

    Bw. Liu Kun pia amesema, ripoti ya kazi ya serikali ya China ya mwaka huu imetangaza mpango wa kupunguza kodi na ada za bima karibu dola za kimarekani bilioni 300, idara za fedha za China zitafanya maandalizi mazuri na kuutekeleza kihalisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako