• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuboresha zaidi mazingira ya biashara ili kuvutia uwekezaji wa kimataifa

    (GMT+08:00) 2019-03-07 20:07:05

    Kutokana na ripoti ya kazi iliyotolewa na serikali ya China kwa bunge la umma, China imeorodhesha kuboresha mazingira ya biashara kuwa moja ya kazi kuu kumi za serikali. Wakati uhusiano wa kibiashara duniani unakuwa wa utatanishi na kubadilika mara kwa mara, hatua hiyo si kama tu itahamamisha maendeleo ya uchumi wa China, bali pia itanufaisha wawekezaji wa kimataifa.

    Tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China ulipofanyika, China imetekeleza hatua mfululizo za kuboresha mazingira ya biashara ikiwa ni pamoja na kupunguza sekta zinazopigwa marufuku uwekezaji kutoka nje, kurahisisha utaratibu wa usimamizi wa serikali na kuinua kiwango cha huduma. Kwa mujibu wa ripoti ya mazingira ya biashara iliyotolewa mwezi Oktoba mwaka jana na Benki ya Dunia, nafasi ya China duniani ilipanda kutoka nafasi 78 hadi 46.

    Mwaka huu China itaendelea kuboresha mazingira ya biashara, ili kukabiliana na changamoto mbalimbali. Kwa mfano itaendelea kupunguza sekta zinazopigwa marufuku uwekezaji kutoka nje, na kodi na malipo ya makampuni kwa karibu dola karibu bilioni 300 za kimarekani. Pia China imeahidi kuyatendea makampuni ya ndani na ya nje kwa usawa katika shughuli mbalimbali.

    Katika mambo ya sheria, ikiwa nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, China inaharakisha kulinganisha sheria za ndani na sheria za kimataifa. Serikali ya China imekabidhi mswada wa Sheria ya Uwekezaji wa Nje kwa mkutano wa Bunge la Umma unaofanyika sasa. Kwa mujibu wa mswada huo, hakimiliki za ubunifu za wawekezaji wa nchi za nje zitalindwa kikamilifu, na hawatalazimika kukabidhi teknolojia zao kwa China.

    Mazingira mazuri ya biashara yanaweza kuvutia uwekezaji wa kimataifa kwa wingi. Mwaka jana, ingawa thamani ya jumla ya uwekezaji duniani ilipungua, lakini uwekezaji wa kimataifa ulioingia nchini China uliongezeka kwa asilimia 3 ikilinganishwa na mwaka 2017, na kufikia dola bilioni 135 za kimarekani, isipokuwa sekta za benki, hisa na bima. Wakati huo huo, idadi ya makampuni mapya ya nje iliongezeka kwa asilimia 70.

    Rais Xi Jinping anaona mazingira ya biashara yanaweza kuboreshwa zaidi bila ukomo. Ikiwa nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, China bado haijafikia kiwango cha juu zaidi duniani katika mazingira ya biashara. Hivyo inatakiwa kuhimiza mageuzi na kufungua mlango zaidi. Mwaka huu, serikali ya China itayapa maeneo ya biashara huria madaraka zaidi ya kujiamulia katika kufanya mageuzi na uvumbuzi, na kuyawezesha kuboresha zaidi mazingira ya biashara. Hatua hiyo itahimiza uchumi wa China kuungana zaidi na uchumi wa dunia, na kuifanya China ivutie zaidi uwekezaji wa kimataifa katika siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako