Ripoti kutoka kwa idara ya soko la kahawa ya Nairobi inaonyesha kuwa gunia la kilo hamsini la kahawa liliuzwa kwa shilingi 15,600 tu ikilinganishwa na 18,700 za awali.
Bei ya kahawa kote duniani imekuwa ikishuka tangu mwezi Novemba mwaka jana ilipofikia senti 113 na baadaye senti 98.
Na taakwimu kutoka kwa ofisi kuu ya kahawa zinaonyesha kuwa wakulima walipata dola milioni 41 kati ya Otkoba na Januari mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |