• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: KCB kufungua tawi China

    (GMT+08:00) 2019-03-07 20:10:25
    Benki ya KCB ya Kenya imesema kuwa itafungua ofisi nchini China ili kupunguza gharama za biashara kati ya nchi hizo mbili.

    Afisa mkuu wa idara ya fedha kwenye benki hiyo Lawrence Kimathi amesema kwa sasa wanajadili maafisa wa serikali ya China na kwamba ofisi hiyo itafunguliwa mwezi Juni.

    Kimathi amesema pia KCB China itasaidia wafanyabiashara wa Kenya na Afrika Mashariki kulipia bidhaa zao kwa kutumia fedha za nchi zao.

    KCB ina matawi nchini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini.

    Aidha benki hiyo imesema itaanza kutoa huduma ya kubadilisha fedha za China yaani Yuan kwenye matawi yake yote kabla ya mwisho wa mwaka hu.

    Amesema lengo la kuwa na Yuan kwenye KCB ni kupunguza gharama za ununuzi kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako