Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Kilimo na Ushirika, Japhet Hasunga, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya Mradi wa USAID -NAFAKA, na kampuni ya kimataifa ya Marekani ya uzalishaji na usambazaji mbegu na viuatilifu (Corteva).
Waziri Hasunga alisema wakulima wamekuwa wakipata hasara baada ya mazao yao kuharibiwa na mafuriko, ukame pamoja na viwavijeshi licha ya kutumia gharama kubwa ya uzalishaji.
Alisema serikali imeona changamoto hiyo na kwamba iko kwenye mkakati wa kuanzisha bima ya mazao kwa wakulima ambayo itakuwa mkombozi wakati wa majanga hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |