• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi asisitiza nia thabiti ya kuendeleza mapambano dhidi ya umaskini

    (GMT+08:00) 2019-03-08 08:58:18

    Rais Xi Jinping wa China ametoa wito wa kuwa na nia thabiti ya kuendeleza mapambano dhidi ya umaskini, wakati miaka miwili tu imebaki kwa China kufikia lengo lake la kutokomeza umaskini kabla ya mwaka 2020.

    Rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China na mwenyekiti wa kamati kuu ya kijeshi ya Chama, amesema hakuna kurudi nyuma hadi ushindi kamili utakapopatikana.

    Rais Xi amesema hayo wakati aliposhiriki kwenye mjadala na wajumbe kutoka mkoa wa Gansu kwenye Mkutano wa pili wa Bunge la awamu ya 13 la umma la China unaofanyika hapa Beijing.

    Rais Xi amesema China imepata maendeleo makubwa kwenye mapambano magumu dhidi ya umaskini katika miaka iliyopita, na pia imefungua ukurasa mpya kwenye historia ya binadamu ya kupambana na umaskini. Amesisitiza kuwa lengo la kutokomeza umaskini ni lazima litimizwe kwa wakati kama ilivyopangwa.

    Akifafanua vigezo vya kuwaondoa watu kwenye lindi la umaskini, rais Xi amesema wananchi hawatakiwi kuwa na wasiwasi kuhusu chakula na mavazi, huku wakiweza kupata elimu ya lazima, huduma za kimsingi za matibabu na makazi salama.

    Rais Xi amesisitiza kuwa tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na urasimu vinakwamisha juhudi za kupambana na umaskini, na kusema hatua thabiti zinatakiwa kuchukuliwa kuondoa hali kama hiyo, kwenye vita dhidi ya umaskini.

    Rais Xi ameziagiza kamati za chama na serikali katika ngazi zote kubeba majukumu yao kwenye mapambano magumu dhidi ya umaskini, na kutaka juhudi zifanywe kwa wakati kuondoa mienendo isiyofaa kwa maofisa, na kuanzisha kampeni maalumu za kupambana na ufisadi na utendaji mbaya kwenye vita dhidi ya umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako