• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China aeleza sera ya diplomasia ya China na uhusiano kati ya China na nchi za nje

    (GMT+08:00) 2019-03-08 17:37:26
    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing amekutana na wanahabari, na kujibu baadhi ya maswali nyeti kuhusu sera ya diplomasia ya China na uhusiano kati ya China na nchi za nje. Kwa mara nyingi, Bw. Wang Yi amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi nyingine kulinda kithabiti hali ya pande nyingi na mfumo wa kimataifa unaoongozwa na Umoja wa Mataifa.

    Mkutano wa Pili wa Baraza la wakuu la ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda mmoja, Njia moja" utafunguliwa mwezi Aprili hapa Beijing, ambapo Rais Xi Jinping wa China atahudhuria ufunguzi wa mkutano huo na kutoa hotuba. Bw. Wang Yi amesema,

    "Mkutano huo wa pili utakuwa na mambo matatu maalumu, kwanza idadi ya wakuu wa nchi mbalimbali wanaotazamiwa kuhudhuria kwenye mkutano huo imezidi ile ya mkutano wa kwanza. Pili, maelfu ya wajumbe kutoka sekta mbalimbali kutoka nchi zaidi ya mia moja watahudhuria mkutano huo. Tatu, makongamano 12 ya kuhimiza ushirikiano na mkutano wa kwanza wa wafanyabiashara itafanyika, na kuweka jukwaa kwa ajili ya ushirikiano wa sekta za viwanda na biashara. "

    Alipojibu swali kuhusu uhusiano kati ya China na Marekani, Bw. Wang Yi amesema, mwaka wa maadhimisho ya miaka 40 ya uhusiano wa kibalozi wa China na Marekani ni mwaka muhimu kwa pande hizi mbili kufanya majumuisho kuhusu mambo yaliyopita na kupanga mambo ya baadaye. Kuhimiza kwa pamoja kuendeleza uhusiano kati ya China na Marekani ulio wa uratibu, ushirikiano na utulivu, hayo ni maoni muhimu ya pamoja waliyofikia marais wa nchi mbili China na Marekani, ambayo yanatakiwa kuwa mwelekeo wa juhudi za pamoja za watu wa sekta mbalimbali wa nchi hizi mbili.

    "Uzoefu tuliopata ni kwamba ushirikiano utanufaisha pande mbili, na mapambano yatadhuru kila upande. Kama tunapanua ushindani, hakika utapunguza nafasi ya ushirikiano. Tunatumai kuwa Marekani itelewana na China, kutimiza kunufaishana wakati zinapojiendeleza. "

    Bw. Wang Yi alipojibu swali kuhusu hali ya Peninsula ya Korea, amesema China siku zote inashikilia msimamo wa kutimiza lengo la kutokuwa na silaha za nyuklia katika peninsula ya Korea. Kama maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili yataendelea bila kusita na mwelekeo hautabadilika, lengo la kuifanya peninsula iwe sehemu isiyo na nyuklia hakika hatimaye litatimizwa.

    "Njia ya kutatua suala hilo ni kutunga kwa pamoja mpango wa kutimiza peninsula ya Korea isiyo na silaha za nyuklia na kujenga utaratibu wa amani wa peninsula hiyo. Umuhimu wa China hautabadilika. Katika hatua ifuatayo, China itashirikiana na pande nyingine, kutoa mchango kwa ajili ya lengo lililowekwa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako