• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: KCB elimu ya usimamizi wa fedha

    (GMT+08:00) 2019-03-08 19:19:19
    Benki ya KCB Tanzania imetoa elimu ya usimamizi wa fedha, uendeshaji wa biashara na sheria za kodi kwa wafanyabiashara mbalimbali mkoani Arusha.

    Wadau mbalimbali katika sekta ya utalii wakiwamo wafanyabiashara walikutanishwa, ambapo sehemu ya kwanza ilikuwa mahususi kwa wateja wa KCB wapatao 250.

    Aidha, sehemu ya pili katika mafunzo hayo yalihusu wakazi wengine wa Arusha kupata elimu ya huduma za kibenki kutoka kwa wataalamu wa KCB.

    Akizungumza wakati wa kufungua semina hiyo, Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa KCB, Christine Manyenye, alisema wamefanya juhudi mahususi za kuwaleta wadau kama Tanzania National Parks Agency (TANAPA), Mamlaka ya Mapato (TRA), kwa nia ya kujadiliana jinsi ya kutatua baadhi ya changamoto na kupata njia muafaka za kuendeleza sekta ya utalii nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako