• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wachimbaji Tanzanite watakiwa kusajili mikataba

    (GMT+08:00) 2019-03-08 19:19:39
    Wachimbaji wa madini ya tanzanite nchini Tanzania, wametakiwa kusajili mikataba ya uchimbaji wanaoingia na raia wa nje kwenye Wizara ya Madini.

    Ofisa Madini Mkazi wa Simanjiro, Daudi Ntalima, aliyasema hayo wakati akizungumza na wachimbaji wa madini ya tanzanite mji mdogo wa Mirerani.

    Alisema mikataba yote wanayoingia na wageni inapaswa kusajiliwa wizarani na maelezo yatatolewa ofisini kwao.

    Aliongeza kuwa wamiliki wa migodi wanapaswa kupewa utaratibu wa kusajili mikataba hiyo na serikali ikague kubaini namna watakavyonufaika na uwekezaji huo wa wageni.

    Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (Marema), Justine Nyari, alisema suala hilo watalifikisha kwa wachimbaji wote ili kuhakikisha mikataba yote ya uwekezaji inajulikana na kufikishwa ofisi ya madini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako